Pages

Sunday, June 21, 2015

Aya ya Leo - Ayatul Kursi

Hii Aya waislamu tunashauriwa kuisoma kila siku, ukiisoma usiku, Allah anakuteulia mlinzi kukulinda usiku kucha na mabaya yote mpaka asubuhi. Na asubuhi pia ukiisoma, unapewa mlinzi wakukulinda mpaka usiku.

Mtume Muhammad(S.A.W) alisema, " Yule mwenye kuisoma hii aya baada ya kila sala, basi kifo ndo kinachomzuia yeye kuingia peponi."

Basi tujitahidi kuihifadhi hii aya.
 Ayatul Kursi - Miracles of Quran - Ustadh Nouman Ali Khan
 1. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye
hai.Msimamia mambo yote milele. 
2. Hashikwi na usingizi wala kulala. 
3.Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. 
4.Ni nani huyo awezaye
kuombea mbele yake bila ya idhini yake? 
5.Anayajua yaliyo mbele yao na
yaliyo nyuma yao.
6. wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi
wake, ila kwa atakalo mwenyewe. 
7.Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; 
8.Na wala haemewi na kuvilinda hivyo. 
9.Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye
Mkuu
(Qur'an 2:255)

No comments:

Post a Comment