Pages

Saturday, January 31, 2015

Choo na Sinki Pamoja

Katika kupita pita zangu google, nikakutana na hii system ya kuweka sinki na Choo kwenye system mmoja.

Yaani namaanisha hivi
Na hivi..
Yaani hii system inafanya kazi hivi. Uki Flush choo baada ya kulitumia, maji masafi yanatoka kwenye hicho kibomba. Wewe una nawa zako na sabuni, unasepa. 
Maji yataendelea kutoka mpaka tank la maji ya ku flush yakijaa ndo maji yataacha yenyewe.  
Yale maji uliyo nawai mikono pamoja na maji mengine masafi ndo yataenda kwenye tank, kutumika ku flush choo. Yaani hamna cha kushika bomba la maji wala nini, ni FULL BACTERIA FREE.
Sasa kama unaona itakuwa tabu watu kusimama chooni na kunawa hapo hapo, unaweza pia kuchagua design hiyo hapo chini.
Au hii hapa

Unanunua dude zima kama lilivyo hapo juu, na kwenda kupachika tu kwako, of cause fundi bomba anahitajika. 
Yaani the choices are endless. Mie ndo naona, wenzetu wa Japan walikuwa wakiitumia hii system long time toka mwaka 1956.
Jamani kila nyumba iwe na hii system.
Mtume alituambia, msipoteze maji, hata kama unatia udhu kando ya mto wenye maji mengi.
The Prophet said, Do not waste water, even if you perform your ablution on the banks of an abundantly-flowing river.
Weekend Njema Wadau!




No comments:

Post a Comment