Pages

Thursday, December 18, 2014

Msomi wa Leo - Sh. Nurdin Muhammad ahmad aka Sh.Nurdin Kishki

Sheikh Kishki ni mzaliwa wa Dar-Es-Salaam, Tanzania. Ni sheikh kwenye Msikiti wa Vetinari uliokuwa Dar-Es-Salaam. Alisoma dini chini ya sheikh Ibrahim, Sheikh Mohamad, Sheikh Harun, Sheikh Abdul kadr na baadae akamalizia kusomea dini Al-Azhar sharif Misri.

Mwaka 1999 Sheikh alihitimu kuhifadhi Qur'ani, na akashinda mshindi wa Kwanza kwenye  mashindano ya Qur'ani ya kimataifa nchini, na wa pili mwaka wa pili. Sheikh pia alishwahi kushiriki kwenye mashindano ya Qur'ani Misri na Iran.

Alifungua madrasa yake ya kwanza, Madrasatul Iqra(mtaa wa mkamba, Changombe), na pia alifundisha madrasa ya abubakar sadiq(mtaa wa temeke, karibu na eneo la sokota). Baada ya zile madrasa kufungwa,  alianzisha Madrasa ya Istiqama maeneo ya temeke.

Sheikh ametoa Mawaidha ya Dini mikoa 16 ya Tanzania(mbeya, Iringa, Singida, Rukwa(Sumbawanga na vijiji vyake),Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mikoa ya Pwani). Nje ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mozambique, Imarat (Dubai), Oman na Saudi Arabia.

Sheikh katengeneza video nyingi za dini, na pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya kiislamu Al-Hikmah Education Center.

Msikilize mwenyewe akikuelezea historia yake na changamoto mbali mbali alizopata kwenye safari zake za dini.

Mwenyezi Mungu Amlinde na Amzidishie Elimu ya Dini na ya Dunia.

1 comment: