Pages

Wednesday, September 10, 2014

Msomi wa Leo - Dr.Abdul Rahman Ibn Abdul Aziz as-Sudais


Amezaliwa Februari 10 mwaka 1962 Bukayriyah, Saudi Arabia. Ni Imam wa msikiti mkuu wa Makka, Saudi Arabia. Sheikh alishika Quran nzima akiwa na miaka 12. Sheikh alipata Shahada ya kwanza kwenye Sheria ya kiislamu kutoka chuo kikuu cha Riyadh mwaka 1983, na Shahada ya pili kwenye Misingi ya Kiislamu kutoka chuo cha Sheria cha Imam Muhammad bin Saud Islamic University mwaka 1987, na shahada ya tatu kwenye Sheria ya kiislamu kutoka chuo kikuu cha Umm al-Qura mwaka 1995, wakati anafanya kazi kama profesa msaidizi, baada ya kufundisha chuo kikuu cha Riyadh. Sheikh ana mke moja ambaye ni Fahda Ra'uf.

Msikilize mwenyewe sheikh akiswalisha taraweh mwaka huu siku ya nne ya Ramadhani.

No comments:

Post a Comment