Pages

Wednesday, June 25, 2014

Perween Saeed

Perween ni mwenyeji wa mji wa Surjani Karachi, Pakistan. Ni mama wa nyumbani mwenye miaka 53, na mwanzilishi wa Kampuni ya Mama Ntilie Khana Ghar. Ana cheti cha Shahada ya kwanza kutoka chuo cha PECHS, na Shahada ya pili cha Uandishi wa Habari, kutoka Chuo kikuu cha Karachi, Pakistan. Ana mume na watoto wawili wa kike.

Mwaka 2002, ilitokea habari ya mama aliyeua watoto wake wawili sababu alikuwa hana uwezo wa kuwalisha, hii ilimshtua Perween, na kumfanya kujituma kusaidia maskini aliokuwa akiwaona kila siku, ndo hapo akapata wazo la kuanzisha shirika lake lakusadia kuwalisha maskini.

Kampuni yake ya Khana Ghar, alianzisha nyumbani kwake, akipika Roti na Mchuzi na kuwauzia watu kwa bei ya chini. Kwa Rupee 3 (Tshs.51.27), unapata Roti moja kubwa haswa ya kujitosheleza na bakuli la mchuzi.

Kwanini asifanye bure? mwenyewe anasema hakutaka watu wasio na uwezo wategemee vyakula vya bure, mtu inabidi aifanyie kazi kula yake ndo atakuwa na uchungu nayo.

Sasa hivi analisha karibia watu 2000 kwa siku mchana na jioni, na menu yake ni roti kila siku, na kila siku hubadilisha mboga, mchuzi wa choroko, mchuzi wa mboga, mchuzi wa mbaazi, ila jumapili wanapika mchuzi wa nyama. Alianza kwa kupika mwenyewe, sasa ameajiri mama wa kupika mchuzi, na roti zinapikwa na vijana watatu. Robo ya mapato yake inatoka kwa wateja, nyingine inatoka kwake, ndugu majamaa na marafiki, na wasamaria wema. Alianza na moja sasa ana tatu.
 

Mwezi wa Ramadhani anapata misaada mingi kutoka kwa watu, inawasadia kutoa mgao wa vifurushi wa vyakula bure kwa wanaohitaji. Kila kifurushi kina vyakula vifuatavyo:
Kilo 2 za Dengu
Kilo 2 za Mafuta na samli
Kilo 10 za Unga wa Ngano
Kilo 3 za Sukari
Paketi 1 ya majani ya chai
Robo Kilo ya Pilipili hoho, Giligilani, Binzari na Ukwaju
Kilo 5 za Mchele
Kilo 1 za Choroko nyeusi, choroko za manjano, tende, chumvi, maziwa ya unga na chupa ya sharbaat
Na Eid Zake Je?

Ooh She throws the grandest parties in the poorest of neighborhoods!
  
Pia kampuni yake husaidia wanafunzi wasio na uwezo kununua vitabu vya shule, nguo za shule, sanda, na pia husaidia kuchangia mabibi harusi na harusi zao kwa wale wasio na uwezo. Perween anasema, kila siku hua anatafuta jinsi ya kusaidia jamii. 

Watch her story below.
The video is in English

Inspired Yet?

source: khanaghar.org

No comments:

Post a Comment