Pages

Sunday, April 13, 2014

Huduma ya Windows XP Kwishniiiiiiii


Haya wadau wa mambo ya teknolojia. Microsoft walitangaza mwisho wao kutoa huduma kwenye operating systems yao ya Windows XP ilikuwa tarehe 8 April mwaka 2014.

Kama una computer ya nyumbani au kazini kwako, amabayo system yake inaendeshwa na Windows XP, basi hili swala ni lako. Kila wiki, Microsoft hutoa updates kwenye computer yako, hizi updates kwa kawaida zinakuwa na security fixes. Microsoft systems zake kwa vile ni nyingi duniani, zina shambuliwaga zaidi na ma hackers. Ni vizuri kuhakikisha unazi update mara kwa mara, ili uweze kulinda files zako, na passwords zako ukiingia mitandaoni.

Microsoft sasa hivi ana Windows 7 na Windows 8.1, unaweza ku update computer yako, lakini computer lazima iwe na atleast dual core processor, iweze kufanya kazi na speed nzuri.


Nenda hapa uka upgrade Operating system yako.


No comments:

Post a Comment