Pages

Thursday, January 2, 2014

Msomi wa Leo - Sheikh Yusuf Muhamed Seif Simbano

Alhamdullilah! Tumeuona mwaka mpya wa 2014. Basi tuanze mwaka huu na wasomi wetu wa dini, na leo tunarudi nyumbani kwa Sheikh Yusuf Muhamed Seif Simbano.

Sheik Yusuf Simbano amezaliwa mwaka 1963 Mwanga, Tanzania. Ni Imam mkuu wa msikiti wa Mitungi Buguruni Malapa Dar. Sheikh alihitimu msaafu akiwa mdogo kwenye chuo cha Sheikh Hatibu Msemo huko Mwanga, na akaendeleza elimu yake ya dini na kiarabu Dar, katika chuo cha Almarkas Zulislamiyu Imisriyu kwa muda wa miaka mitano, hichi chuo kiliwekwa msingi na marehemu J.K.Nyerere. Alipomaliza hapo, akienda kumalizia elimu yake Misri kwenye Chuo Kikuu cha Al-Azhar, akachukua shahada yake ya dini utaalamu kwenye Hadithi.

Sheikh alisha fanya kazi ya kufundisha na Bakwata, na pia alisha fundisha Chuo cha Abdillah bin Abas, na Chuo cha Jamia Nuria hapo nyuma. Sheikh anaongea kiswahili na kiarabu vizuri.

Sheikh Simbano ana mke mmoja na watoto watatu, wawili wa kiume na wakike mmoja. Mke wake Sakina binti Ismaili, alianzisha kituo cha watoto yatima kinachoitwa Mwana Orphans Center kilichokuwa Dar. Walianza na watoto watano, wakapata wafadhili waliowasaidi kukiendeleza na kukiendesha kituo kikakuwa mpaka sasa kina watoto 50.

Talk about a power couple who do good and know how to live in this world. Kuna somo hapa ya aina ya mke au mume unataka awe partner wako wa maisha. Partner atakaye kuinua uwezo wako kikamilifu uweze kuendelea kwenye maswala ya Dini na Dunia, au atakaye kurudisha nyuma na kukupotosha?

Msikilize mwenyewe Sheikh anakwambia Fadhila za kumfurahia Mtume Muhamed(S.A.W) na mazazi yake.

Mashallah! Mwenyezi Mungu Amzidishie yeye na familia yake, hekima, elimu ya dunia na dini. Na awaekee nuru yake kwenye familia nzima ya Sheikh Simbano.

No comments:

Post a Comment