Pages

Friday, June 21, 2013

Usiku wa nisf Shaban - The Night of Salvation

Huu usiku una angukia kati ya tarehe 14 na 15. Maulamaa wengi wamependekeza kufanya ibada usiku huu kutokana na hadithi ya Mtume Muhammad(S.A.W). Baada ya Swala ya Maghrib au Isha ni vizuri kusoma Suratul Yasin, dua na useme "La Hawla walaa Quwwata illa Billahil-aliyil Azeem" (maana yake: Hakuna Kudura wala Nguvu isipokuwa ya Allah -There is neither might nor any power except with Allah). Tumuombe Mwenyezi Mungu atu samehe madhambi yetu na waliotangualia mbele yetu, atuepeushe na majanga ya dunia, atuzidishie imani, atupe afya njema, Amani duniani na atufungulie milango ya kheri hapa duniani na Akhera.Pia ni vizuri kufunga tarehe 13, 14, 15 wa mwezi wa Shaban (Juni 22,23 na 24). Kama huwezi basi jitahidi kufunga tarehe 15 baada ya usiku wa ibada kwa ajili ya maombi yako, na In Shaa Allah Mwenyezi Mungu atakufanyia mambo yako yawe mepesi.

Ibn Majah alisema: Mtume Muhammad(S.A.W) aliwaambia, usiku huu Allah atasema, " Kuna mtu yoyote anaye omba msamaha nimsamehe, mtu yoyote anayeomba msaada nimsaidie, mtu yoyote mwenye dhiki nimpe faraja, usiku kucha mpaka Alfajiri.

(English translation of the Hadith)
The prophet Muhammad , said that during the night of 15th of Shaban, Allah will say "is there any person repenting so that I forgive him, and any person seeking provision so that I provide for him, and any person with distress so that I relieve him, and so on until dawn." reported by Ibn Majah.

No comments:

Post a Comment