Pages

Monday, June 10, 2013

Mwezi wa Shaban 2013

Leo tunamalizia mwezi wa Rajaab, ambao ni moja ya miezi 4 mitukufu iliyo tajwa kwenye Qurani na Hadithi, na Kesho tunaukaribisha mwezi Shabaan. Mtume Muhammad(S.A.W), alikuwaga akifunga mwezi wa Shabaan kasoro siku chache za mwisho. Tujitahidi kufanya ibada sana mwezi huu, na kufunga kujitayarisha mfungo wa Mwezi ujao ambao ni Ramadhan. Nawaacha na hii hadithi ya Mtume Mohammed(S.A.W), Allah apokee ibada zetu na maombi yetu na atu epushe na majanga ya Dunia.

Ummul Mu'mineen 'Aishah (r), alisema, "Mtume Muhammad , alikuwa akifunga siku nyingi za Shaban. Nikamwambia, 'Ewe Mtume wa Allah, kwani Shaban ndio mwezi uupendao kufunga?' Akamjibu, "Mwezi huu Allah anatoa orodha ya watu watakao kufa mwaka huu. Kwahiyo, ningependa kifo changu kije wakati nikiwa nimefunga."

No comments:

Post a Comment