Pages

Monday, May 6, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AWAJULIA HALI MAJERUHI WA MLIPUKO JIJINI ARUSHA

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.…
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa Kanisa hilo.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha.
(PICHA NA OMR)

No comments:

Post a Comment