Pages

Friday, March 29, 2013

Jengo laporomoka Dar Mjini

Jamani Ijumaa ndio imeanza hivi. Jengo laporomoka mjini mtaa wa Indira gandhi pembeni na msikiti wa ma Shia. Inasemakana mpaka sasa watu wawili wamefariki na wengine wamejeruhiwa, jengo lilikuwa halija maliziwa kujengwa.

Project ilikuwa Joint venture ya NHC. Hao Lucky Construction na SOU consult na ma engineers wao wote bomu. They got some explaining to do.
Duh! Hali Inatisha
  
Yaani, jengo liliziba barabara. Hii ni hatari sana.





Kwakweli hizi habari ni nzito. Je hili jengo lingekuja kuanguka wakati limeshafunguliwa? Wanaitaji kuchunguza, material walizotumia kujengea hili jengo, na kucheki supplies zote na suppliers wao. Kisha wapitia majengo yote mapya yaliyo jengwa kutumia hivi vifaa vya hawa suppliers, zote ziwe inspected upya.
Inna lilahi waina illahi raj'iun. Kwa Mwenyezi Mungu ndio tunapotoka na ndio marejeo.Mwenyezi mungu awalaze waliotangulia mahali pema peponi. 
Picha nimetoa kwa Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment