Pages

Wednesday, January 2, 2013

Juma Kilowoko AKA Sajuki atuacha

(1985-2013)
Jamani mbona mwaka unaanza hivi tena. Nimesikita kupata habari ya Juma Kilowoko Almaaruf kwa Sajuki msanii wa filamu za bongo amefariki dunia alfajiri ya tarehe mbili kwenye hospitali ya Muhimbili. Rajabu Amiri mkuu wa chama cha waongoza filamu wilaya ya ilala, ametoa habari kuwa sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.


Wote tunakumbuka jinsi Sajuki alivyougua vibaya baada accident yake ya pikipiki, ambaye ilisabibisha mchumba wake kwa sasa ni mke wake Wastara kukatwa mguu moja,na yeye kusumbiliwa na mambo mengi ikiwemo uvimbe tumboni. Mwaka 2011 watu tulichangishana akaenda India kutibiwa. Kumbe hakupona kabisa, na juzi juzi hapa Arusha, alianguka kwenye stage. Na habari ni kwamba alikuwa arudi tena India kwa matibabu zaidi. Duh! kweli huyu Kaka aliteseka.
"Ugonjwa ni kama kituo cha polisi, kuingia rahisi kutoka na hela". Haya maneno mazito aliyanena mwanzoni wa mwaka 2012 alivyorudi kutoka India.


 Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)
To him we belong and to him we shall return. May Allah forgive his sins and accept him into his heaven.

Source: IPP Media

No comments:

Post a Comment