Pages

Friday, June 28, 2019

Aya ya Leo - Habari (The Message)


Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo tunamuongoza tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoza kwenye Njia Iliyo Nyooka.

And thus We have revealed to you an inspiration of Our command. You did not know what is the Book or [what is] faith, but We have made it a light by which We guide whom We will of Our servants. And indeed, [O Muhammad], you guide to a straight path (Qur'an 42:52)
Jumaa Mubarak Wandugu!


Aya za Leo - Nijengee Mnara - Firauni (Build for me a tower..-Pharaoh )

.. build for me a tower that I may attain the means of access to the heavens, then reach the God of Moses..-Pharaoh
Na Firauni akasema:" Ewe Haman! nijengee mnara ili niweze kupata njia." "Njia za mbinguni ili nikamuone Mungu wa Musa; na kwa yakini ninamjua kuwa ni muongo tu (huyo Musa, lakini nataka kukuonyesheni na nyinyi)." Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake na akazuiliwa njia(ya haki); lakini vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu.

And Pharaoh said: O Haman! build for me a tower that I may attain the means of access. The means of access to the heavens, then reach the god of Musa, and I surely think him to be a liar. And thus the evil of his deed was made fairseeming to Pharaoh, and he was turned away from the way; and the struggle of Pharaoh was not (to end) in aught but destruction. (Qur'an 40: 36-37)
Ijumaa Njema!

Friday, June 21, 2019

Aya ya Leo - Dua (Prayer)


Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.

My Lord! Forgive me and my parents and him who enters my house believing, and the believing men and the believing women; and do not increase the unjust in aught but destruction! (Qur'an 71:28)
Jumaa Mubarak!

Tuesday, June 18, 2019

Egypt's former president Mohamed Morsi dies: State media



Inna lillahi waina illahi rajiun.
Mwenyezi amsamehe madhambi yake na amlaze mahali pema peponi.

Monday, June 10, 2019

Hadithi ya Leo - Mapovu ya Bahari (Sea foam)


Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume wa Allah alisema, Yoyote anayesema,
'Subhan Allah wa bihamdihi,' 
Mara mia moja kwa siku, atasamehewa dhambi zake zote atakama zilikuwa nyingi kama mapovu ya bahari. 

Narrated Abu Huraira:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "Whoever says,
'Subhan Allah wa bihamdihi,' 
one hundred times a day, will be forgiven all his sins even if they were as much as the foam of the sea. (Bukhari 6405)

Friday, June 7, 2019

Aya ya Leo - Uumbaji (Creation)


Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake.

Allah begins creation; then He will repeat it; then to Him you will be returned.
(Qur'an 30:11) 
(Ijumaa Njema Wadau)

Tuesday, June 4, 2019

Makkah Live HD | قناة القران الكريم | بث مباشر |

Makkah Live wakijitayarisha kuswali swala ya Eid Al Fitri na wakifanya takbir.

Hadithi ya Leo - Dhawabu Mia (One Hundred Good Deeds)


Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume wa Allah alisema, "Yoyote anayesema: 
" La ilaha illal-lah wahdahu la sharika lahu, lahu-l-mulk wa lahul- hamd wa huwa 'ala kulli shai'in qadir 
(Hakuna Mungu ila Allah pekee, bila Mwenzie. Yeye ndio Mmiliki, na Mwenye sifa zote, na Mwenye Nguvu juu ya kila kitu)," 
mara mia moja, atapata dhawabu sawa na mtu anayeachia watumwa kumi, na dhawabu mia moja itaandikwa kwenye hesabu zake, na dhambi mia zitafutwa kwenye hesabu zake, na itakuwa ngao yake kutoka kwa shetani siku hiyo mpaka usiku wake, na hamna atakayeweza kumzidi zaidi ya yule anayetenda mema zaidi yake.


 Narrated Abu Huraira:
Allah's Messenger (ﷺ) said," Whoever says: 
"La ilaha illal-lah wahdahu la sharika lahu, lahu-l-mulk wa lahul- hamd wa huwa 'ala kulli shai'in qadir 
(There is no god but Allah, alone, without partner. His is the sovereignty, and His the praise, and He has power over everything)," 
one hundred times will get the same reward as given for manumitting ten slaves; and one hundred good deeds will be written in his accounts, and one hundred sins will be deducted from his accounts, and it (his saying) will be a shield for him from Satan on that day till night, and nobody will be able to do a better deed except the one who does more than he." (Bukhari 6403)

Tukumbuke kufanya sunna ya kwenda kuutafuta Mwezi wa Iddi.